21/04/2026
Kuanzia tarehe 7 Aprili miaka 32 iliopita mpaka katikati ya mwezi julai ya mwaka huo wa 1994. Inakadiriwa watu kati ya 800,000 mpaka 1, 000,000 wa jamii ya Kitusi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa na wanamgambo wa Interahamwe wa jamii ya kihutu ya Rwanda katika maeneo mbalimbali.
Hili ni somo na funzo la kuoenesha chuki ya jamii moja dhidi ya nyingine hasa ya wachache inavyoweza kugeuka maafa na janga lenye kuacha maumivu ya kudumu kwenye mioyo ya Wahanga.
Isijirudie tena!!
Roho mbaya na chuki ya kikabila huwa tabia na kuenea kwa wengi na baadae hugeuka utamaduni.
Tena wakati wa mauaji hakukuwa labda Mwami wa Watusi na au wa Wahutu au wa Watwa. hakukuwa Mfalme wala Chifu. Ilikuwa ni Jamhuri pekee tena bila hata viongozi wa kimila. Pia Wakoloni weupe walichochea chuki na ubaguzi wa kikabila katika kile ambacho tangu zamani wenzetu hao waliamini katika Utadaraki wa Kimbari "Racial Superiority".
Chuki ikizidi huwa haina macho, haina kwao.
Mwanaadamu aliyetoka utu na utashi sahihi wa akili kumuua mwanaadamu mwenzake isivyo haki kwasababu tu ana utamaduni, muonekano, asili na utambulisho tofauti na wa kwake.
Chuki haikuangalia Uafrika, weusi wala ukaribu. Na hii ndiyo maana halisi ya unyama.
Isitokee tena!!
Isijirudie tena!!
Iwe somo!!
Kauli za kusema sisi sote ni waafrika zisituhadae rangi haitoshi kuwaunganisha watu. Bali utu, kuvumiliana na kuheshimu utofauti wa utambulisho wa kihistoria na kitamaduni wa kila jamii.