13/07/2026
Customer wengi wanapitia changamoto kwa sababu ya kuangalia label kuliko packing.
Mtu anakupigia simu akuulize k**a uko na nguo ya label fulani. Unamwambia iko, halafu anasisitiza, "Nataka hiyo hiyo label." Hapo ndipo shida inaanza.
Mimi k**a muuzaji najua hii label inaweza kuwa ilikuwa inatoa nguo safi zamani, lakini kwa sasa quality yake imebadilika. Wewe k**a customer umeona mtu akifungua bale ya hiyo label na ikatoka poa, sasa unaamini kila bale ya hiyo label itakuwa safi. Ukweli ni kwamba si hivyo.
Mara nyingi huwa najaribu kumshauri customer, lakini kwa sababu customer is always right, anaamua kuchukua label aliyoitaka. Mwishowe anapata nguo ambazo hazimfurahishi.
Ndiyo maana huwa nasema ni muhimu kusikiliza ushauri, hasa kutoka kwa watu wanaokutakia mema. Mimi niko kwenye hii industry kila siku. Naona labels zote, nasikia maoni ya wateja kila siku, na najua ni zipi zinafanya vizuri na zipi quality yake imeanza kushuka.
Kampuni nyingi zikianza huwa quality yao ni nzuri. Lakini demand ikiongezeka sana, mara nyingi wanajaribu kuongeza supply haraka, na hapo quality inaweza kushuka.
Somo la leo ni hili: Usinunue bale kwa kuangalia label. Nunua kwa kuangalia packing.
Na k**a nimekuambia packing fulani imeharibika, usiogope kubadilisha label. Hiyo ushauri unaweza kukuokoa pesa nyingi.
Kwa hii ni siri muhimu sana:
Mitumba bales haziamuliwi na label... zinaamuliwa na packing.
Good day! 🙏