29/05/2018
NGUVU YA CPU
Unajua kua ubongo wako ni k**a computer? Yaaan una ram, rom, hard disc na processor...
Computer kile utakachoicommand ndicho kinachofanyika yaaan ukitaka computer yako iwe maalum kwaajili ya video games then all the apps zitakua hivyo, ukitaka iwe kwaajili ya movie then itajaa movies, ukitaka iwe kwaajili ya u-DJ then itajaa kila aina ya nyimbo zote duniani. Yaaan kwa ufupi unachotaka ndicho kinachokua, ndio maana unasikia kuna core i3, core i5, core i7 na zingine means chaguo ni lako... The same applies to your mobile phone. Ila amini kuna watu hawajui matumizi sahihi ya hivi vitu hujikuta anakua na core i7 kwaajili ya kuingia Facebook na social media zingine 🤷🏽♂🤷🏽♂ hajui jaman usimlaumu
Sasa basi ubongo wako upo hivyo hivyo na kile unachotaka kiwepo kichwani kinakua katika hali ya kawaida maishani mwako. Hivi unategemea ubongo wako uwe umeujaza mambo ya akina Diamond na Ali Kiba sijui Mobetto mara Wema Sepetu utegemee kabisa utakua na uwezo wa kuchangia mada katika seminar ya katiba??? Thubutuuuuu
Jibu la swali la kwanini Wa Africa ni masikini ni simple tunajaza bongo zetu na unwanted materials k**a mipira, udaku, ngono, siasa chafu n.k then tunakosa muda wa kuweka mambo ya uchumi na maendeleo katika bongo zetu
Simple task angalia WhatsApp yako aina ya magroup uliyopo, nenda Facebook angalia aina ya groups na pages ulizolike, nenda Instagram angalia aina ya watu uliowafollow na unaowasearch mara kwa mara then nenda google yako bonyeza pale juu kulia nenda kwenye history angalia aina ya vitu unavyosearch mara kwa mara utapata jibu kwanini bado upo hapo
My friend you are who you are because of what you feed your brain, anza kubadili aina ya vitu hivyo na futa k**a unavyodelete file kwenye computer utaanza kuona kumbe ubongo wako una space kubwa tu ya kuingiza vitu vya msingi
Cha mwisho ni hiki movie moja ukiiweka kwenye computer yako inachukua nafasi ya kuanzia MB 600 na kuendelea ila kitabu kimoja kukiweka huko hakizidi hata MB 10, yaaan movie moja ni sawa na Vitabu 60, jiulize kwenye computer/simu umejaza nini cha msingi cha kushibisha ubongo wako vizuri?...Maamuzi ni yako, chagua sahihi ili usije kujuta baadae.
Siku njema wapendwa
Mr Mtenga
TAECO LTD