Abandélwa

Abandélwa Davies official page ���������

24/11/2021


Monday mood😅
23/08/2021

Monday mood😅

14/02/2021

1. VALENTIN est mort par l'amour
2. ROMEO est mort par l'amour
3. JACK dans leTitanic est mort par amour
4. SAMSON dans la bibible est mort par amour
5. HERCULES le héros grec est mort par amour
6. JESUS fils de Dieu est mort par amour
Où sont les femmes dans cette liste?
*n'achetez aucun cadeau de Sain Valentin ce 14 Février juspu'à ce que les femmes nous donnent le nom de 5 femmes mortes par amour, Trop c'est Trop

25/08/2020

X 134
Muandishi…………………………………………..EDDAZARIA G.MSULWA (Genius Author)
Wasiliana nami……………………………………0657072588/0768516188/0742334453(WhatsApp)
Age……………………………………………………….18+
Website
Haki zote zime hifadhiwa, hairuhusiwi kunakiliwa, ku forward au kupost kwa mtu yoyote, group, blog, website au kuirekodi pasipo idhini ya muandishi. Endapo uta k**atwa kwa kosa hilo, sheria kali zitachukuliwa dhidi yako. Asante na ungana nami katika kisa hichi cgha kusisimu.
@2019

ILIPOISHIA
“Nani wewe?”
“Kijana wako hapa”
“Nani?”
“Nahitaji uweze kufika hapa kituoni”
“Bwana sasa hivi nimepumzika na mke wangu hivyo siwezi kuja. Nipigie asubuhi”
“Kweli”
“Kweli nini sasa, wewe ni kiziwi au?”
Mzee huyu alifoka pasipo kujua ana ongea na nani. Akakata simu, nikampigia simu tena huku nikiwa nime weka loud speaker.
“Nimesema nimelala sitaki usumbufu pumbavu wewe?”
Watu wote wakastuka namna jinsi mzee alivyo nitukana laiti k**a angejua ana zungumza na nani nina hisi hata huo usingizi wenyewe ungekuwa umesha kwisha.

ENDELEA
(AIISSII YOU KILL ME CHAPTER FOUR(Killer) inazidi kusonga mbele. Wahi sasa ujiunge kwenye group WhatsApp 0657072588 kwa sh 4000/= tu.
Karibu sana)
“Sawa muheshimiwa. Endelea kulala”
Nikakata simu huku watu wote wakinitazama. Nikatabasamu kuwaonyesha kwamba sijakasirika ila kusema kweli moyoni mwangu huyu mzee ameivuruga saa.
“Bibi yangu yupo wapi?”
Nilimuuliza mlinzi huyu uso wake ukatawaliwa na huzuni kubwa kiasi cha kunifanya nianze kuhisi mabaya juu yake.
“Yupo wapi?”
“Walimfukuza kazi miezi kadhaa iliyo pita. Na kutokana hakuwa na pakwenda na maisha yake yalikuwa ni hapa basi alifariki dunia kwa huzuni na mawazo. Madaktari walisema mishipa ya kichwani ilipasuka na kusababisha kifo. Hicho ndio nilicho kisikia kutoka kwa madaktari”
Habari hii ikanistua kiasi cha kujihisi moyo wangu ukichomoka. Kusema kweli bibi alikuwa ndio k**a mama yetu kwemye hichi kituo kwani ni watu wengi sana ambao tumelelewa na yeye hususani mimi ambaye aliniokota nikiwa nimetupwa mtaroni. Machozi yakaanza kuniolenga lenga huku hasira ikizidi kunipanda.
“Nani alimfukuza?”
“Bodi ya kituo”
“Kwa nini?”
“Bibi alikuwa akiwauliza juu ya pesa zilizo tolewa kwa ajili ya ujenzi na wao wakamuona ni k**a msumbufu hivyo wakamfukuza.
“Watu wa bodi ya kituo un awajua?”
“Namjua mkuu tu ila wengine siwajui”
“Kaburi la bibi lipo wapi?”
“Njoo nikuonyeshe”
Tukaondoka na mlinzi huyu hadi kwenye eneo la makaburi ya watu walio wahi kuishi kwenye kituo hichi. Eneo hili la makaburi lina zikwa watu wote walio pita kwenye hichi kitio cha Makete. Tukafik katika kaburi la bibi ambalo limefukiwa k**a la watu wengine na halijajengwa hata kwa tofauli moja. Msalaba wenyewe umeliwa na mchwa kiasi kwamba tumeukuta umeinama.
“Walishindw akulijengea?”
“Sijui mkuu”
Mzee Kamweni alizungumza kwa huzini.
“Nashukuru mzee”
Tukarudi kwenye eneo yalipo magari.
“Mzee endelea na majukumu yako tuta onana asubuhi”
“Sawa”
Mimi na W***y tukaingia ndani ya gari na kumkuta Cauther na mwanaye wakiwa wamesha lala.
“Uta wafanya nini?
W***y aliniuliza kwa sauti ya upole mara baada ya ukimya wa k**a dakika tano kupita bila ya kuzungumza chochote.
“Sijui W***y”
Nilizungumza huku machozi ya hasira yakinibubujika.
“Asubuhi ndio watanitambua”
“Kina nani hao baby”
Cauther alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama usoni mwangu.
“Ehee?”
“Kina nani watakukoma”
“Washenzi hawa wamekula zile pesa na walimfukuza bibi kazini ikiwa miaka yake yote amejitoa kufanya kazi kituoni hapa. Na sijui ni nani alitengua nafasi yake na kuamua kumfukuza.”
“Ohoo walimfukuza bibi wa watu?
“Si kumfukuza tu ila kwa sasa bibi hatupo naye duani”
“Nini!!?”
Cauther aliniuliza kwa msisitizo.
“Ndio hivyo bibi hatupo naye duniani alisha fariki dunia na hapa nimetoka kulitazama kaburi lake, wameshindwa hata kulijengea kweli?”
“S…sa. Kwa nini wamfukuze wakati aliniambia nimletee mjukuu kabla hajafa jamani”
Cauther alizungumza huku machozi yakimlenga lenga.
“Sasa Nadia ata muanaje bibi yake?”
Cauther aliendelea kuzungumza kwa huzuni kubwa na kunifanya nizidi kujawa na hasira.
“Nitadili nao hawa washenzi”
“Sasa alifariki kwa tatizo gani?”
“Mawazo yalipelekea mishipa ya kichw akupasuka na akafariki dinia”
“Jamani sasa walimfukuza ili wanufaike na nini?”
“Alikuwa ana ona uchungu wa pesa za kijana wake jinsi zinavyo fanyiwa upumbavu na wapuuzi wale. Sasa nita dili nao hawa shenzi sana”
Usingizi haukuninyemelea hadi kuna pambazuka. Nikashuka ndani ya gari huku nikiwa nimevaa koti kubwa sana, kwani barini ni kali kiasi cha kufanya ukungu kuwa mwingi sana. Nikamfwata mzee Kamwende getini na kumkuta akiwa amelala.
“Shikamoo mzee”
“Marahaba”
“Ohoo pole nime kustua ulikuwa umelala?”
“Ndio, usingizi ulinipitia bwana. Niambie kijana wangu?”
“Naweza kupata wapi vafaa vya ujenzi asubuhi hii. Nataka nikajengee lile kaburi”
“Vifaa vinauzwa madukani ila kwa sasa sidhani k**a maduka yamefunguliwa”
Nikatazama saa yangu ina onuyesha sasa ni saa kumi na mbili na dakika ishirini.
“Tuna weza kutembea hadi madukani?”
“Ndio hakuna tatizo”
Tukanza kutembea taratibu kuelekea madukani.
“Kwenye umri wako huu una tarajia kufanya kitu gani kingine tofauti na ulinzi?”
Nilimuuliza mzee Kamwene huku tukitembea kwa miguu.
“Mimi kila kazi nafanya, japo nina umri mkubwa ila ni mkak**avu.”
“Sawa, hivi uan watoto wangapi?
“Kwa sasa amebakia mmoja wa k**e yupo mkoani Shinyanga”
“Amebakia mmoja una maana gani?”
“Nilikuwa na watoto wanne. Watatu walifariki kwa nyakati tofauti tofauti na amebakia huyo mmoja wa k**e na ameolewa huko Shinyanga”
“Aise pole sana”
“Nimesha poa”
“Sasa yeye ana fanya kazi gani?”
“Ni mwalimu wa shule ya msingi”
“Ohoo sawa sawa”
Tukafika eneo la madukani na kukuta duka moja tu likiwa ndio limefunguliwa.
“Kwa nini wana chelewa kufungua maduka”
“Kipindi hichi cha baridi huwa watu wengi huchelewa kuamka.”
“Wana uza vitu gani kwenye lile duka?”
“Nguo nyuo”
Tukalisogelea duka hili.
“Habari mama”
“Sal..ama”
Mwana mama huyu akapata kigugumizi kidogo huku akinitazama. Nikakatazama kwenye moja ya ukuta wake nikaona amening’iniza picha yangu huku ikiwa na maanidhishi ya raisi wa jamuhuri ya muungano ya Tanzania Eddy Jr. Akaitazama picha ile kisha akanitazama na mimi.
“Una mabushori?”
“Eehee”
“Hembu nionyeshe”
Mama huyu akaniletea mabushori yenye rangi tofauti tofauti.
“Samahani baba”
“Bila samahani”
“Wewe ndio raisi Eddy?”
Mzee huyu akanitazama, nikamkanyaga kidogo kwa maana sitaki watu watambua kwamba nipo hapa na isistoshe nimesha toka madarakani na hata nguvu yangu ya mamlaka ya kiuongozi imepungua kwani nikiwa k**a raisi mstafu kuna baadhi ya mambo huwa siwezi kuyafanyia maamuzi zaidi ya raisi aliyopo mdarakani.
“Hapana mama yangu?”
“Kweli baba, mbon auna fanana na raisi wangu kipenzi”
“Una mpenda ehee?”
“Sana nina mpenda sana raisi huyu. Kwanza ni kijana, pili ni mzuri, tatu ana chapa kazi na ana misimamo k**a muasisi wa hii nchi”
“Una gloves zile ngumu?”
“Hapana zipo za kitambaa pekee”
“Sawa mama yangu. Bushori hili sh ngapi?”
“Ni shilingi elfu tano baba”
Nikafungua wallet yangu na kutoa noti za shilingu elfu kumi mbili na nikamkabidhi”
“Hiyo nyingine uta kunywa supu”
“Asante sana baba yangu. Nashukuru sana baba yangu, asante sana”
“Mimi ndio huyo kwenye picha”
Mwana mama huyu akatoka dukani kwake na akanikumbatia kwa furaha huku akiliwa kwa furaha.
“Mama usimuambie yoyote k**a nipo hapa”
“Haki ya Mungus into muambia yoyote”
“Kweli?”
“Ndio baba yangu. Nafurahi leo nimemkumbatia raisi, ohoo asante Mungu wangu”
Mwana mama huyu alizungumza kwa furaha. Nikamuachi.
“Ili watuw asikujue ina bidi uvae miwani na hilo bushori”
“Kweli ehee?”
“Ndio”
(AIISSII YOU KILL ME CHAPTER FOUR(Killer) inazidi kusonga mbele. Wahi sasa ujiunge kwenye group WhatsApp 0657072588 kwa sh 4000/= tu.
Karibu sana)
“Nimeona miwani hapa dukani kwako”
“Ndio zipo baba ngoja nikupatie”
Mwana mama huyu akanichagulia moja ya miwani na akanikabidhi.
“Hiyo nimekupa k**a zawadi baba yangu”
“Niseije nikawa nina kuingizia hasara?”
“Hapana baba yangu wewe chukua tu ni zawadi yangu”
Nikavaa miwani hii nyeusi pamoja na bushori hili lenye rangi nyeusi.
“Ni duka lipi wana uza vifaa vya ujenzi”
“Kuna lile la mchaga pale ila hajafungua, nahisi muda si mrefu ata fungua”
“Nashukuru sana mama yangu”
“Karibu sana baba”
“Asante”
Tukaondoka dukani hapa na kuingia kwenye moja ya mgahawa wa kawaida.
“Mzee wangu kula chochote unacho hitaji”
Nilizungumza huku tukikaa kwenye moja ya bechi. Tukaagizia supu na chapati. Kwa jinsi nilivyo vaa hapakuwa na mtu aliye nijua na uzuri ni kwamba nimekuja peke yangu bila walinzi laity ningekuwa na walinzi watu wangefahamu.
“Nasikia gari la Msenga ni milioni stini?”
Mmoja wa wateja aliye kaa na wezake wawili kwenye meza moja wakipata kifungua kinywa alizungumza.
“Duuu Milioni stini?”
“Ndio milioni stini lile gari”
“Kwa mtu k**a Msenga amezitolea wapi pes azote k**a si wizi”
“Si kuna mradi pale kituoni nasikia ni wawafadhili kutoka Ujerumani, wamechakatua pesa na wakagawana watu wa juu juu na Msenga akavuta zile pesa”
“Asiee k**a kanunua gari la milioni stini ina maana wameingiza kiasi gani?”
“Mmmm wala sijui kwa kweli ila ina onyesha ni pesa nyingi sana”
“Msenga ndio nani?”
Nilimnong’oneza mzee huyu.
“Ni mkuu wa kituo uliye zungumza naye jana usiku”
“Okay”
“Ila jamaa nasikia kajenga sana kwao, kajenga saa kwao huko”
“Wee”
“Nasikia jamaa sasa hivi ni tajiri kutokana na kile kituo”
“Ila sijui rushwa ita isha lini pale”
“Ila jamai tuyaachei maisha ya watu. Sisi tuendelee kupambana na hali zetu”
“Ila kweli”
Watu hawa wak**aliza kula na wakaodoka eneo hili. Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa nikalipa kisha tukatoka ndani hapa. Tukaelekea katika duka la Mchaga, nikanunua vitu vya kujengea kaburi na tukaanza safari ya kurudi kweye kituo taratibu. Gari nyeusi aina ya BMW ikatupita kwa kasi.
“Gari ya mkuu huyo”
Mlinzi alizungumza huku gari hii ikitupotea kweye uwepo wa macho yetu. Tukafika katika kutuo, walinzi wangu wakatupokea mizigo hii. Nikaitazama gari ya mkuu wa kituo hichi ambayo ni mpya kabisa.
“Huyo mpuuzi aliye ingia na gari yupo wapi?”
Nilimuuliza mlinzi wangu.
“Ameelekea ofisini”
“Mlke wangu”
“Bado yupo kwenye gari”
Nikatembea hadi kwenye gari, nikafungua mlango na kumkuta Cauther, mama mkwe, shemeji pamoja na mtoto.
“Shikamoo mama”
“Marahaba, haabri yaw ewe”
“Salama saa mama yagu. Muna edneleaje?”
“Tumeamka salama, ila baridi kali sana huku”
“Yaani shem huku ni full kutetemeka”
“Poleni, ila by saa tano sita hivi baridi ita isha kajua katatoka toka”
“Aisee”
“Vipi mke wangu”
“Safi mume wangu. Ulienda wapi?”
“Huko kwenye mji kununua nunua baadhi ya vifaa. Nataka kwenda kujengea lile kaburi”
“Ohoo una kwenda lijengea sasa hivi?”
“Hapana baadae ila acha kwanza niwanyooshe hawa wapumbavu”
“Sawa”
“Kina nani hao mwanangu?”
Mama mkwe aliniuliza.
“Usijali mama yangu. Munahitaji nini?”
“Tuna hitaji kuoga maji ya moto kidogo kwa maana kwa hii baridi hapana jamani”
Nadia aliulizugumza na kunifanya nitabasamu.
“Acha niwaandalie mazingira”
“Sawa”
Nikaondoka eneo hili.
“W***y yupo wapi?”
“Amekwenda ofisini kwa mkuu wa kituo”
“Sawa”
Nikaelekea katika ofisi ya mkuu wa kituo hichi cha watoto yatima. Nikamkuta bwana Msenga akiwa amekaa kwenye kiti chake huku W***y akiwa amekaa kwenye kiti kinacho tazamana na bwana Msenga. W***y akanipa ipad yake.
“Kaka hiyo ndio pesa iliyopo kwenye akaunti ya kituo hichi chote”
Nikajikuta macho yakinitoka kwani akaunti ya kituo ina kiasi cha shilingili elfu sabani na mbili tu jambo ambalo ni la kushangaza sana kwani kwa shilingi elfu sabini na mbili haiwezi kuendesha maisha ya watoto walipo kwenye kituo hichi wala kuwalipa mishahara wafanyakazi wa kituo hichi.
(AIISSII YOU KILL ME CHAPTER FOUR(Killer) inazidi kusonga mbele. Wahi sasa ujiunge kwenye group WhatsApp 0657072588 kwa sh 4000/= tu.
Karibu sana) ITAENDELEA
Haya sasa, rushwa ya wazi wazi ina onekana ina fanywa kwenye kituo hichi cha watoto yatima je ita kuwaje kwa bwana Msenga na timu yake? Usikose kuungana nami tena katika sehemu ya 135.

😂😂😈😄
13/02/2020

😂😂😈😄

08/02/2020

Davies official page

09/01/2020

HADITHI: SAYARI YA GUTTA
MTUNZI: Amani H. Kigoye
SIMU: +255766416862
WhatsApp: +255766416862
Fb: Aman Kigotyme
Email: [email protected]
SURA YA NNE: SHIMO LA ALMASI
SEHEMU YA SITA(06).

Hatimae mwezi uliisha tangu tufike katika ardhi ya hii sayari ya GUTTA mambo yalikua yanenda k**a tulivyopangilia lakini mwenzetu DANIEL hali yake ilikua bado haijaimalika bara bara kwani alikua bado hawezi kutembea muda wote huo alikua anashinda amelala. Kwa mara ya kwanza tuliweza kuandaa safari ya kwanza kwa ajili ya uchunguzi wa kugundua mahali yanapopatikana madini ya URANIAM, na safari yetu ilikua twende hadi kwenye misitu iliyokua ikionekana kwa upande wa mashariki.
Safari iliandaliwa na kila kitu kilikua kipo sawa na waliotakiwa kwenda katika zoezi hilo ni mimi, MARIAM, Zakia, GODIAN na ISSA LUMBWE na wote tulikua tumeshajiandaa kwa ajili ya hiyo safari. Stoo ilifunguliwa iliyokuwepo nyuma ya ile roketi na ilitolewa gari ndogo ya wazi ya kijeshi aina ya lendi kruza iliyo wazi, tulipakia kila kitu ndani ya gari na kila mmoja alikua ana siraha yake aliyoiona yeye inamfaa.
Wote tulijipakia ndani ya gari na Zakia Sadiki alik**ata usukani wa gari na safari ikaanza kuelekea kunakotakiwa kwenda. Nikiwa nimekaa pembeni ya MARIAM huku nikiwa nimeshikilia ule mkufu niliokabidhiwa na mke wangu uliokuwa unaning`inia muda wote shingoni mwangu, niliushika na kujikuta nikijiongelea moyoni “ soon nitarudi my cute wife na mateso yako yatafikia mwisho…kila siku na pambana kwa nguvu zangu zote ili nije nikusaidie mke wagu”. “dokta vipi…? Mbona unaonekana unamawazo mengi…?” GODIAN aliniuliza huku akiwa anageukia nyuma na kutuangalia tulipokuwa tumekaa mimi na MARIAM. Nilishtuka toka katika lile dimbwi la mawazo na kumuangalia kwa jicho kali GODIAN, na alijishuku na kuangalia mbele huku akijisemea kwa sauti ya chini chini “ mmh…!!! Watu na mawazo yao wasije wakatutafuna hali ya kuwa tunatembea..”. “ kumbe unalitambua hilo na kukaa kimya?” Zakia alimjibu GODIAN huku macho yakiwa mbele na mikono ikiwa imeshikilia vizuri uskani wa gari yake.
Baada ya masaa taklibani mawili kupita hatimae tulifanikiwa kuwasili katika ile misitu minene tuliyokua tumepanga kuifikia mwanzo wa safari yetu. Zakia aliegesha gari pembeni ya msitu na kila mmoja alishuka huku akiwa amebeba begi lake mgongoni lenye vifaa vyake vya kazi tayali kwa utafiti kuanza. “mh!!” GODIAN alijikuta anaguna huku akiwa analitengeneza begi lake mngongoni na kukoki bastola yake ndogo na kuiweka kiunoni mwake kwa mbwembwe zote. “vipi na hiyo silaha kuna nini?” ISSA alimuuliza GODIAN huku akifunga mlango wa gari. “nothing afande” alimjibu na kuanza kuingia msituni kumfata MARIAM alipokuwa anaelekea, na wote tukaanza kufata msafara tukizama msituni kwa ajili ya kuanza kazi iliyotupeleka eneo lile.
Ulikua ni msitu mnene na ulikua na miti mirefu iliyokuwa na matawi yenye majani marefu tena matawi yake yaliweza kufungamana vizuri kuanzia juu ya shina hadi chini, iliyosababisha msitu uonekana uliofungamana sana na kuleta kiza ukiwa kati kati ya ile miti. Ilikua ni kazi ngumu sana kupenya katikati ya ile miti lakini tulifanikiwa kupenya penya kwani ISSA na MARIAM walikua na vifaa maalumu vya kukatia matawi ya ile miti na kuyaangusha chini. Tukiwa watu makini huku Zakia akiwa na kifaa maalumu kilichokuwa kinatafuta eneo ambalo yale madini ya URANIAMU yanapatikana. “vipi hakuna dalili yoyote” nilimuuliza Zakia huku nikinyenyua tawi la mti lililokua mbele yangu na kulitupia pembeni, “hakuna ila naamini tutakapozidi kusogea mbele mambo yatakua mazuri” Zakia alinijibu huku akikiangalia kile kifaa kwa umakini na kusonga mbele. “sasa si tunaweza tukawa tunazunguuka bila mafanikio yoyote na msitu huu ulivyo mnene hivi tutaweza kukumbuka njia tulioijia”, “ hakuna kitu k**a iko dokta kwanza hapa si tuna kifaa kinacho onesha mahali ambapo kambi ilipo kwa hiyo haina haja sana ya kujali kwa hilo” Zakia alinitoa wasi wasi na huku tukiendelea na kazi mule msituni. “duh! Huu msitu wazee mbona unanipa mashaka” GODIAN akiwa na MARIAM mbele na wao walijaribu kupiga soga, “ acha uwoga wako k**anda”. “ sio uwoga kapteni, hivi wewe huoni huu msitu ulivyo au?”, “ mbona mimi naona kawaida sana”, “ ok hakuna shida k**a unaona ni kawaida…tuendelee na kazi k**anda wangu” alimjibu huku akimuangalia MARIAM usoni na kutabasamu.
Mambo yalizidi kuwa magumu maana tulijikuta tunazunguuka kwa muda wa masaa taklibani mawili bila mafanikio mule msituni, wote tukajikuta tumechoka na kukaa chini ya mti mkubwa ulikuwemo mule msituni na kuanza kutafakali kwa kina. Nilijitupia chini na kutupa begi langu chini huku nikipiga fundo moja la maji na kumuangalia MARIAM usoni nikionesha kila dalili za kukata tamaa kwa kazi ile tuliyoifanya mule msituni. MARIAM aliniangalia na uso wake ulionesha kila hali ya kuendelea kupambana kwani bado alikua na uhakika na utafiti wake alioufanya kipindi tupo duniani. MARIAM alimuangalia Zakia na kukaa chini huku GODIAN akiwa anajiongerea k**a mwendawazimu, “ mimi nilisema jamani isije tukawa tunakuja kufanya kazi ya bure huku” kila mmoja alimuangalia kwa jicho la husuda na alijikuta akijishuku na kukaa chini. “eee!!... basi waungwana msije mkanivamia nilijaribu kuwakumbusha tu” lakini hakuna hata mmoja aliyemjibu na kwa muda wote huo ISSA alikua yuko kimya na macho yake yalikua hayatulii kila kona ili mradi kuhakikisha usalama wetu unakua uko makini.
Tulikaa eneo lile kwa muda wa dakika 15 bila kupata wazo lolote na kila mmoja alionekana dhahili safari yetu iishie hapa tuanze kurudi kambini, lakini Zakia aliposimama na kusogea hatua tatu mbele kile kifaa chake kikaanza kupiga makelele kikiashilia kwamba kuna eneo lina madini. “ Zakia nini iko kinachopiga kelele?” GODIAN aliuliza huku akikurupuka kutoka pale ardhini na kumfata Zakia alipo. Kabla Zakia ajajibu wote tulikurupuka na kumsogelea alipo na kumtolea macho tujue nini kinachojili, lakini Zakia hakutujibu bali alikusanya mizigo yake na kuanza kuelekea mahali kifaa kinapomuelekeza na sisi bila kuuliza tulimfata nyuma. “ sasa tunaenda wapi….?... mbona hatuelezani jamani…?” GODIAN aliuliza huku akiwa amesimama na begi lake mkononi akitushangaa tunavyoondoka, “ tusubilie hapo hapo tunakuja sasa hivi” MARIAM alimjibu huku akitukimbilia tuliokuwa tunatokomea msituni. “ nyooo…!! Eti tusubilie hapo hapo…mnaumwa nini?” huku akiweka begi begani mbio kutuwahi tulipoelekea.
Tulitembea mwendo wa dakika 30 bila mafanikio huku kile kifaa kikiendelea kupiga kelele kuashilia kwamba tunazidi kulisogelea eneo tunalolikusudia. “ jamani mbona hivi?” GODIAN aliuliza, lakini hakuna aliyemjali na swali lake kwani kila mtu alikua yuko bize kutafuta ni wapi madini yalipo. “ mbona hamnijibu jamani?” alitupa begi chini na kuinama huku akiwa ameshika magoti kuashilia kwamba amechoka kupindukia. “jaamaaaaniiiii eeeeeeh…….!!!!!!” Safari hii alituita kwa sauti kali na akakaa kimya ghafra, “ GODIAN…!!!!!!” MARIAM aligeuka huku akimuita kwa hasira kuonesha sasa tumechoka kelele zake, lakini tulipogeuka wote tulimkuta GODIAN amekaa chini huku akiwa ameyatoa macho pembeni ya kichaka kilichokuwepo nyuma yake. Wote tulipatwa na mshtuka naye ISSA alikoki SMG yake na kuelekea alipo GODIAN lakini alishikwa mkono na MARIAM, “hebu subili kwanza k**anda”. “GODIAN kuna nini?” Zakia alimuuliza huku nayeye akiandaa silaha yake tayali kwa lolote lile. “nothing but…..” alisita na kuokota begi lake kuelekea kwenye kile kichaka, ikatubidi na sisi tumfate ili tupate kujua ni nini alichokiona mwenzetu. Tulipomfikia tu GODIAN alipo wote tulijikuta tukiangaliana usoni tusijue nini chakufanya huku tukiwa tumeachama midomo k**a tumefumaniwa.
Kwa upande wangu sikuweza kuamini nilichokua nakiona mbele ya macho yangu kwani hakikuwahi kuonekana kabla tangu nianze kuishi katika hii dunia. Nilipomuangalia Zakia niliona ana angalia kile kifaa na ghafra kikaacha kupiga kelele kuashilia eneo tulilokuwa tunalitafuta sasa tumeshalipata, “ nazani hapa ndipo tulipokua tunapahangaikia kwa muda mrefu” Zakia aliongea huku akijaribu kutoa majani yaliyokuwepo kwenye kile kichaka. Tulipo jaribu kukisafisha kile kichaka tulikutana na pango kubwa ambalo lilikua lina waka waka kwa vitu vilivyokuwa vimetanda katika kuta za lile pango. “ ni nini?” MARIAM aliuliza, “ that is DAIMOND” ISSA alimjibu MARIAM huku akisogea ndani ya pango kuweza kuziangalia kwa ukaribu ni kweli zilikua ni almasi au macho yalimdanganya.
“ yes ni almasi ndio maana kifaa kilikua kinapiga sana kelele nazani kwa ajili ya hii kitu” huku akiibandua moja wapo iliyokuwa imekaa kwenye jiwe lililokuwepo ndani ya lile pango. “ una…una…unataka kusema hizi…hizi…hizi… ni almasi?” GODIAN alimuuliza ISSA huku akifungua begi lake na kuanza kubandua baadhi zilizokuwepo kwenye lile jiwe. Baada ya kumuona GODIAN anafanya kile kitendo hakuna aliyetaka kupoteza muda kila mmoja wetu alifungua begi lake na kuanza kupakia ndani ya mabegi yetu maana kila mtu alijua sasa umaskini ndio bai bai. Ilikua ni kuchuma almasi na sio kuchimba maana zilitapakaa k**a majani ya muembe, hii ilikua kali maana nyie huko duniani mnahangaika na mitambo kuchimba madini ya almasi lakini sisi huku tulikua tunayachuma tu bila mashaka. Kila mtu ilikua ni kicheko na tabasamu la furaha usoni na kila mtu alitamani kambini kuwe karibu ili awe anaendea mabegi na mifuko ili ajaze na kurundika ndani ya roketi, lakini haikuwa hivyo tulivyotamani.
Kazi ilipamba moto maana kila mtu alishindilia ndani ya begi lake na bado zile almasi zilikua ziko pale pale na tena zilikua zinazidi kumelemeta balaa. GODIAN alikua kashachanganyikiwa kabisa na begi lake lilikua limejaa vilivyo ikambidi awe anaziweka ndani ya mifuko ya kombati yake ya jeshi. Akiwa mtu mwenye kihelehele alijikuta akidakwa mkono na Zakia “watch out…!!! Kamanda” huku akimuonesha mbele yake kilichopo. Tulipo jaribu kuangalia ni nini HAMMAD!!! Lilionekana shimo kubwa lililoenda chini bila kuona mwisho wake na lilitoa mvuke na sauti za ajabu. Wote tulisimama kwanza huku tukishikwa na uwoga na kila mmoja akiwa anatetemeka, lakini kwa upande wa GODIAN alijikuta anatetemeka hadi kijasho chembamba kikimtiririka, “ oooh oooopssiii ni ni ni…..nini tena?” aliuliza huku akiwa anatetemeka kwa uwoga.
Tukiwa tuna jiuliza lile shimo ni la nini ghafra GODIAN alitutaka tukae kimya tusikilize kwa umakini, “hebu sikilizeni kwanza” huku akitega sikio kuelekea kwenye lile shimo kwa umakini. “ mbona hatusikii kitu?” nilimuuliza huku nikimuangalia usoni. “jamani hamsikii sauti yoyote tofauti na huu muungurumo humu shimoni”. Wote tulitega sikio lakini hatukufanikiwa kusikia chochote ndipo ghafra kwa sauti ya ukali Zakia alipiga kelele akitutahadharisha tulale chini, bila kupinga tulijikuta tukijitupia chini bila kujali nini kinachotaka kutokea. Ile tunalala tu chini lilitoka kundi kubwa la ndege wasiojulikana wenye langi nyeusi na macho mekundu tena walitoka kwa kelele ambazo hatukuwahi kusikia zile sauti katika maisha yetu yote.
Akati tukiwa tunalala chini ndege mmoja alimpitia begani Zakia na kumchana bega, kile kitendo kilimfanya Zakia apige kelele za maumivu na kuanguka chini. ISSA alikoki bunduki yake na kuanza kutupa risasi zilizowapata baadhi ya ndege walioanguka chini kwa fujo na mmoja wapo alimuangukia GODIAN,kile kitendo kilimfanya apiga kelele na kumrusha Yule ndege pembeni. MARIAM alipoona ISSA anawapa zawadi wale ndege ilimbidi nayeye aanze kumwaga risasi huku akituamuru tumsaidie Zakia pale chini, wale ndege walikua wakitoka kwa fujo na walikua wakubwa wenye midomo mirefu iliyochongoka vilivyo na kwa jinsi walivyo maumbo yao kwa duniani sikuona aina yoyote ya ndege ambao wangefanana na hawa ndege.
Nilinyenyuka haraka haraka huku nikiwa na umakini mkubwa juu ya wale ndege wasije wakanijeruhi na mimi nikiwa naelekea alipokua ameangukia Zakia , bila kusubilia nilianza kumburuza Zakia ili nimtoe eneo lile asije akashambuliwa zaidi na wale ndege wa ajabu. Mkono wangu wa kulia nilikua namvuta Zakia hali ya kuwa mkono wangu wa kushoto nikiwa nimeibeba ile siraha aliyokuwa nayo Zakia huku nikiwa natoka nje ya lile pango na wenzangu wakiendeleza mapambano dhidi ya wale ndege wa ajabu. GODIAN aliliwahi begi lake na kulivaa mgongoni tena akilifunga vilivyo kifuani kwa kutumia mikanda iliyokua ikining’inia na ndipo alipochomoa bastola yake na kuanza kuwashambulia wale ndege wa ajabu. Msitu mzima ulilindima sauti za risasi na sauti za wale ndege wakilalamika kwa hasira huku wakiwa wanatoka ndani ya lile shimo lilikuwemo katika lile pango na kukimbilia juu ya ile miti mirefu.
Nikiwa niko makini nikimpa huduma ya kwanza Zakia huku nao wenzangu wakiendelea kuwapunguza wale ndege, ndipo nilipotupa jicho mbele yangu nilikutanisha macho yangu na ndege mmoja aliyetua huku akinisogelea kwa hasira. Nikiwa bado nimeduwaa nisijue cha kufanya, Yule ndege alitanua mabawa yake na akaanza kuja kwa kasi mahali nilipo ili aweze kunishambulia. Nilianza kutetemeka na kuitafuta bastola yangu ndogo niliyoiweka kiunoni lakini kabla sijaifikia Yule ndege aliruka na kuja usoni mwangu akitanguliza miguu yake na kutoa kucha zake ndefu nyeusi ili anitoboe macho yangu. Nilijikuta nafumba macho yangu na ghafra nilisikia mlio wa risasi na kushtukia kitu kikiniangukia usoni, nilikurupuka pale chini huku nikifumbua macho yangu niweze kujua nini kilichotokea, ndipo nilipokutana na MARIAM akiwa amenyoosha siraha yake kuashilia kwamba amemuuwa Yule ndege na kuokoa maisha yangu. "Kuwa muangalifu doctor!" Mariam alinitahadhalisha kisha akaendelea na yake.
Nilimuangalia Zakia na kuanza kuona ule mkono wake ukianza kubadilika rangi na kuwa na rangi ya kijani taratibu kuonesha kwamba wale ndege walikua wana sumu kali na inayosambaa kwa kasi mwilini. Nilichukua kamba ya kiatu changu na kuifunga karibu na bega la ule mkono uliojeruhiwa na Yule ndege ili sumu isiendelee kusambaa kwa kasi na kuleta madhara sehemu zingine za mwili wa Zakia. Kisha nilijikaza na kumnyenyua pale chini huku nikiwaamuru wenzangu tutoke eneo lile maana ilikua ni hatari kwa maisha yetu. “ inatubidi tufanye haraka tuondoke eneo hili hawa ndege wanasumu kali” niliwapigia kelele na kila mmoja alianza kurudi kinyume nyume huku akiendelea kuwashambulia wale ndege waliokua wanajaribu kutufata. Alikuja ISSA na kumvua begi Zakia na kumsaidia kulibeba huku mimi nikiendelea kujikokota nikimsaidia Zakia kutembea kwani nguvu zilianza kumuishia na hata usoni alionekana kupauka na midomo kumkauka. Hatimae wale ndege waliacha kutoka katika lile pango lakini wengi wao walikua wametanda juu ya ile miti, na safari hii ilikua shida kwao kutuona kwani tulikua tupo kati kati ya ile miti mirefu iliyofungamana vilivyo. Wale ndege walitapakaa juu ya ule msitu na wakawa k**a wingu la mvua tena kwa ile rangi yao nyeusi unaweza kusema mvua itanyesha muda si mrefu.
Wenzangu waliacha kumimina risasi na tukaanza kuitafuta njia ili tuelekee sehemu tulipoegesha gari yetu, safari hii tulisaidiana na MARIAM kumkokota Zakia ili tupate kuwahi kutoka eneo lile. Tukiwa tuko makini tukitafuta njia ya kutokea lakini ghafra tulimsikia GODIAN “ hey hey guys listen” huku akisimama na kutega sikio vizuri. Wote tulisimama na kumgeukia GODIAN aliyekua nyuma yetu huku tukimuuliza nini kinaendelea, lakini mwenzetu akapiga magoti chini na kulaza kichwa chake chini akitega sikio vizuri ardhini bila sisi kujua anafanya nini. “ inamaana nyie hamsikii chochote kuacha hizo kelele za hao ndege?” alituuliza huku akinyenyuka pale ardhini alipokua amepiga magoti. “ mimi sisikii chochote hebu twendeni jamani tusipoteze muda” ISSA alimjibu GODIAN huku akiukunja uso. Lakini baadae ilinibidi niwaambie wenzangu “ jamani hebu tusimpuuzie”, niliongea hivyo kutokana na kitendo cha mara ya kwanza kule pangoni alituambia hivi hivi na tulimpuuzia wakatokea ndege wa ajabu. Huku kichwani nikianza kugundua uwezo wa masikio na ngozi ya GODIAN kuwa inaweza ikahisi kitu chochote hata kikiwa mbali. Tukiwa bado tunabishana ndani ya ule mzozo mara tulisikia kishindo kikubwa huku kikiambatana na mtetemeko uliotushtua na kutaka kuanguka. “ nini iko jamani?” GODIAN aliuliza huku akilikagua begi lake mgongoni k**a liko salama au limetoboka, hakuna aliyemjibu kwani hakuna hata mmoja aliyeweza kujua ni kitu gani kinachoendelea pale msituni.
Tuliamua kuanza kutimua mbio lakini mimi nikiwa na Zakia wenzetu walituacha ndipo ikambidi ISSA arudi na kuvua mabegi aliyokuwa nayo na kuyaweka chini “ dokta nipe mimi Zakia wewe chukua hayo mabegi na hizo siraha kimbia nazo”, huku akimtwaa Zakia mikononi mwangu na kumtupia begani kwake na kuanza kukimbia nae kuelekea mahali tulipo egesha gari yetu. Lakini hatufika mbali GODIAN alitushtua na kututaka tulale chini kwa haraka, hatukufanya ajizi tulijitupa wote chini, tena bila kuamini wala kutalajia tuliona moto mkali ukiunguza juu ya miti na ngurumo nzito ikifatiwa sambamba na mitetemo iliyo ambatana mfururizo. ISSA alijikuta anamtupa Zakia na akaenda kuangukia kwenye jiwe lililompiga kichwani na kumchana katika paji lake la uso na damu zilianza kumvuja kwa wingi. Tuliangaliana na ISSA bila kujua nini cha kufanya maana tulikua tupo katika wakati mgumu kwa muda ule, “dokta KIGOYE fanya ukamsaidie Zakia….umpe huduma ya kwanza” MARIAM alinipa maagizo huku akitambaa kwa kutumia tumbo lake kulifata begi lake aliloliangusha kipindi alipokua anaruka kukwepa ule moto ambao hatukujua ulikua unatoka wapi.
Haraka haraka nilitambaa hadi mahali alipokua ameangukia Zakia na kuanza kumpa huduma ya kwanza ili niweze kuzuia damu iliyokua ikiendelea kumtoka kwenye jeraha lake, lakini huko upande wa pili moto ulizidi kulindima na kwa muda wote huo hatukuweza kujua ulikua unatokea wapi. Nilifanikiwa kumuhudumia Zakia hadi damu zilikata ndipo nilipoanza kumburuza ili niweze kumtoa eneo lile, maana hali ya hewa ilibadilika ghafra na msitu mzima ulitanda moshi mnene kutokana na ule moto uliokua ukiunguza ile miti. Kwa kuwa hatukua mbali sana na gari yetu nilifanikiwa kulifikia lakini nilishindwa kumuweka mgonjwa ndani ya gari maana nilichokiona nilishindwa kuamini machoni mwangu. Kila siku katika maisha yangu nilikua nasikia tu baadhi ya wanyama kwamba walishawahi kuishi duniani lakini sikuwahi kuwaona, na hata k**a nilishawahi kuwaona basi walikua ni wa kutengenezwa au niliwaona kwenye baadhi ya filamu za kizungu, lakini nilijikuta najionea kwa macho yangu mubashara mnyama aliyefahamika k**a DRAGONI.
Sikuamini kabisa na nilijikuta naishiwa nguvu huku nikimbwaga Zakia chini na kujificha kwenye kichaka kilichokuwepo karibia na gari yetu, na kuanza kumshuhudia anachokifanya Yule mnyama. Alikua ameenda hewani na mwenye shingo ndefu, miguu iliyo shiba vilivyo yaani alikua akipiga hatua moja alifanya ardhi itikisike na kulete tetemeko la ardhi, mwili wake ulifunikwa na ngozi nene yenye magamba k**a ngozi ya mamba, na alikua ana mabawa makubwa yaliyokua akiyachanua na kuyakunja huku akiwa anapiga kelele na kutema moto mkali uliokuwa ukiunguza ule msitu.
Nililala kwa muda huku Yule mnyama akiendelea kutema moto na kupiga kelele za ajabu kile kitendo kilizidi kuniogopesha kwani wenzetu walikua bado wamo mule msituni huku moto ukizidi kupamba moto. Baada ya dakika 15 kupita sikuweza kusikia sauti ya wale ndege wala sauti ya Yule DRAGONI bali nilisikia sauti ya moto tu ukiendelea kuteketeza ile miti. Nilipochungulia tena kumuangalia Yule DRAGONI nilimuona akitanua mabawa yake na kuanza kuyapiga piga kwa hasira kisha akaanza kupaa na kuja eneo nililokuwepo nimejificha mimi na Zakia. Nilirudisha uso wangu na kuuficha katika majani huku nikipata hisia za upepo mkali ukinipuliza mgongoni na nilipotupa jicho la wizi wizi nilimuona Yule mnyama akipita hewani mgongoni kwangu na kuondoka zake. Sikuamini kabisa mpaka pale nilipomuona kwa mbali ametokomea katika milima iliyokuwepo mbali na maeneo yale, ndipo nikanyenyuka na kwenda kumuinua Zakia ambae alikua hajitambui kabisa, nilimuinua kutoka sehemu aliyokuwa amelala kisha nikampandisha ndani ya gari. Nilipomaliza kumpandisha Zakia ndani ya gari niligeuka kuangalia ule msitu jinsi ulivyokua unateketea kwa ule moto, huku moyoni nikijawa na hofu kubwa k**a wenzetu wataweza kutoka salama. Nikiwa naendelea kupakia mabegi ya ISSA, Zakia na la kwangu ndipo nilipoanza kusikia sauti za majani zikisikika kutokea katika ule msitu, nilichukua ile SMG ya ISSA na kuikoki tayali kukabiliana na chochote kitakachotokea. Lakini nilipoangalia kwa umakini niliweza kugundua ni MARIAM akiwa na wenzake wakija huku wakionekana wamechoka hawajiwezi kwa ule moshi uliokuwa umetanda ndani ya ule msitu. Nikaitupa chini ile silaha na kumpokea MARIAM, “ am ok dokta” aliongea huku akikohoa kikohozi kikavu kuashilia ya kwamba moshi ulimuasili. Ndipo nilipomuonaa ISSA na GODIAN na wao wakitokea msituni huku wakiwa wako hoi, niliwa amulu wapande ndani ya gari ili tuanze safari ya kurudi kambini haraka.
“ vipi begi langu liko salama?” ISSA aliniuliza huku akikohoa na kujitupia ndani ya gari, lile swali lilinifanya nitake kucheka lakini ikanibidi nijizuie na kumjibu ISSA “yeah liko salama…mabegi yote nimeyatupia huko nyuma ya gari” huku nikiwasha gari tayali kwa safari ya kurejea kambini. Gari ilishtuka na iliondoka kwa mwendo mbaya hadi nikaacha vumbi nene nyuma likienda kushindana na ule moshi uliokuwa ukitokea katika ule msitu. Sikutaka mchezo maana ilinibidi niwaishe ili niokoe maisha ya wenzangu tena hususani Zakia ambae hali yake ilikua mbaya zaidi ya wenzake. Nikiwa niko makini na uskani wa gari nilitupa jicho pembeni kumuangalia Zakia niligundua tayali alikua ameshazima kabisa, basi ikanibidi niongeze mwendo wa gari ili yasije kutokea mengine. Gari ilifika kwenye bonde na ilijikita na kuwafanya wote washtuke ndani ya gari, kile kitendo kilimfanya hadi Zakia atoe mguno ambao ulianza kunipa imani kwamba nitaweza kuwahi na kuokoa maisha yake. “dokta vipi unataka kutumwaga njiani?” GODIAN aliuliza huku akikaa vizuri huku akishikilia chuma kilichokuwepo pembeni yake. “ sorry k**anda wangu nawahi ili niokoe maisha ya mwenzetu”, “hivi ule moto ulikua unatoka wapi?” aliuliza tena swali lingine “ maana hata nilikua sijui…au wenzangu mlielewa wapi ulipokua unatokea?” GODIAN alizidi kuongeza mzigo wa maswali. “ule moto ulikua unatolewa na DRAGONI” nilinjibu huku macho yakiwa mbele nisije kukosea njia. “dragoni!!!!???” aliuliza kwa mshangao mkubwa huku akiangalia nyuma kana kwamba huyo mnyama anakuja, lakini sikumjibu niliendelea kuendesha gari huku nikiwa na wasi wasi juu ya maisha ya Zakia k**a ataweza kupona kweli kwani ile sumu ilionekana ni kali sana ikishaingia ndani ya mwili wa binadamu na nilipouangalia ule mkono wake niliona ushabadilika rangi na kuwa mweusi na mishipa ya damu ilikua imesimama na kujitokeza katika ngozi yake.
Baada ya masaa kadhaa tuliwasili tena kambini na kupaki gari kwa fujo zote na kuwakuta wenzetu wote wakiwa wamesimama wakitaka kujua ni kipi kilichotusibu maana huo mwendo niliokua nakuja nao ulikua sio wa kawaida. Ile gari ina simama na vumbi zito lilifata nyuma na kuwafanya wote waanze kukohoa na kujifuta futa usoni na wengine wakificha nyuso zao maana ilikua sio kawaida kabisa. Nilishuka na kufungua mlango wa gari alipokua amekaa Zakia na kutaka kumshusha ndani ya gari, “ dokta vipi?” SALVA aliniuliza huku akinisaidia kumshusha Zakia ambae alikua hajitambui kwa muda huo wote. Sikuweza kumjibu bali nilimtaka BITE akaandae vifaa ili tuweze kumuhudumia Zakia haraka iwezekanavyo maana hali yake ilizidi kuwa mbaya. Na wale wengine waliokua ndani ya gari walishuka huku wakiwa bado na mawenge ya ule moto wa kule msituni, kile kitendo kiliwafanya wote wabaki wameduwaa wasijue nini kilichotupata maana wenzangu wote walikua wako na hali mbaya kasoro mimi tu ndiye niliekua niko vizuri.
“ we shall talk letter.. now tunahitaji kuwahudumia kwanza hawa wenzetu wenye hali mbaya tena hususani Zakia kabla sumu haijazidi kuleta madhara mwilini mwake” nilimjibu BITE aliyetaka kujua kipi kilichotusibu. “sumu!!??” aliuliza kwa mshangao mkubwa , “yeah kuna sumu ndani ya mwili wake iliyotokana na ndege wa ajabu tuliowakuta kule msituni” hakuwa na cha kuongea BITE alibaki ameduwaa na kusogeza vifaa ili nianze kumuhudumia Zakia. Niliuangalia ule mkono wenye jeraha kuanzia katika vidole vyake hadi kwenye jeraha lenyewe ndipo nilipogundua kuna kipande cha kucha kimekatikia katika lile jeraha. Hapo hapo ndipo nilipogundua kuwa ni kipande cha kucha cha wale ndege waliokua wakitushambulia kule pangoni. Muda wote huo mimi nikiwa naendelea kumshughulikia Zakia nae BITE alienda kuwahudumia wakina MARIAM na wenzake ili wapate angalau nafuu kutokana na ile hali ya kuvuta moshi mkali uliowafanya wakose oksijeni ya kutosha mwilini.
Niliweza kumfanyia upasuaji mdogo na kuondoa kile kipande cha kucha na kukiweka pembeni ili nikakifanyie uchunguzi wa kina hapo baadae. Nilimsafisha na kumpa dawa za kuzuia ile sumu ili isiendelee kumdhuru huku nikimtundikia dripu ya damu maana alipoteza damu kiasi alipojigonga kwenye lile jiwe kubwa. Nilipomaliza nilitoka ndani ya ile zahanati ndogo nikiwa na kile kipande cha ile kucha na kuingia nacho ndani ya chumba changu na kuanza kukifanyia uchunguzi ili nipate kujua ni aina gani ya sumu iliyokuwemo ndani ya wale ndege.
Hatimae kiza kiliingia nami nikiwa ndio namalizia kufanya uchunguzi juu ya ile sumu ya wale ndege ndipo nilipotoka na kurudi tena kwenye zahanati alipopumzika Zakia na kuanza kuchanganya baadhi ya dawa na kupata mchanganyo wa dawa ambayo ingeweza kupambana na ile sumu iliyokuwemo ndani ya mwili wa Zakia. Nilipomaliza kuchanganya zile dawa nilienda kupima ubora wake na kugundua mchanganyiko uko sawa ndipo nilipo mpa Zakia anywe, kisha nikamwambia apumzike maana kwa mbali fahamu zilianza kumrudia taratibu.
Nilipotoka nje ya roketi niliwakuta wenzangu wote wakiwa wanapiga soga za hapa na pale na kubwa ilikua ni suala lile lililotukuta kule msituni. Nilifika na kukaa kwenye kitu kilichokuwepo karibu na SALVA. “vipi dokta… anaendeleaje?” SALVA aliniuliza huku akinipa kopo la soda ya baridi nipoze koo. “she is fine” nilimjibu huku nikifungua ile soda ya kopo nipate kupoza koo kidogo, “asee poleni sana kumbe kilikua ni kizaa zaa kikubwa mzee” INNO aliongea huku akiniangalia nilivyokua nimechoka. Kwanza nilikata fundo moja la soda kisha nikaweka kopo chini “ ilikua sio mchezo hilo timbwili lake yaaani…… hata sijui nielezee vipi”, “ GODIAN ametupa habari jinsi ilivyokuwa mzee” PILLA aliongea huku akicheka kwa utani. “ acheni tu na bora msikie na sio mkutane na hilo songombingo lake” niliongea huku nikipiga tena fundo lingine la soda. Basi ikawa ni utani na mizaha ya hapa na pale juu ya lile seke seke lililotukuta kule msituni.
“ila akati nafanya uchunguzi juu ya ile sumu ya wale ndege nimegundua pia wanafaida katika maisha yetu” nilipo ongea hivyo watu wote walinitumbulia macho, “ unasemaje dokta!!?” GODIAN aliniuliza huku akinikodolea macho. “nasema hivi ile sumu ya wale ndege inafaida kwetu..” nilisita kidogo na kumalizia ile soda yangu iliyokuwemo ndani ya lile kopo kisha nikaendelea, “ unajua nini…? Sio kuja huku kwa shughuli moja tu bali inatubidi tuwe wabunifu na wagunduzi zaid ya kile kilichotuleta huku”, “unamaanisha nini dokta?” MARIAM aliniuliza huku akiwa ananifatilia kwa umakini. “ hapa najaribu kuwa fumbua macho ya kwamba tunaweza kuitumia hii nafasi tuliyoipata ya kuja huku kwa kuweza kugundua vitu vingi vyenye manufaa kwa binadamu kutokana na vitu au viumbe tunavyokutana navyo huku”. “ sawa mimi nimekuelewa dokta tena sana, sasa vipi kwa hao ndege wenye sumu wanaweza wakawa na faida kwetu angali madhara yake tumeyaona kwa Zakia?” SALVA aliniuliza huku akinipa kopo jingine la soda, “ no no no inatosha” nilimzuia ile soda aiweke pembeni maana nilikua nishatosheka kisha nikamjibu swali lake. “nimesema hawa ndege wanafaida tena sana maana nimeiona sumu yao inaweza kutumika kutengenezea dawa za kuulia wadudu waharibifu na pia ukatengenezea madawa ya kusafishia vyoo na vitu vingine vinavyoendana na hivyo vitu” nilipomaliza kusema hivyo wote walikaa kimya ghafra na kisha nilishangaa wakipiga makofi mazito kuonesha wamekubali yale mawazo yangu.
“ wewe dokta ni jiniazi ndugu yangu” GODIAN aliongea huku akija kunipa tano na kunipigia saluti mbele yangu. “sasa tutawapataje hao ndege?” ISSA aliniuliza ambae muda wote alikua yuko kimya kwani huaga apendi kuongea mara nyingi. “hiyo kazi rahisi sana kwasababu wakati Yule dragoni alipokua anatema ule moto kuna ndege wengi waliungua na walipoteza maisha, sasa pale sisi tunatakiwa kwenda na kuwakusanya wale ndege wote na kuwaleta hapa kambini” nilipumzika kidogo na kumuangalia GODIAN maana alikua anajambo anataka kusema, “ sikia dokta hivi kwa hali ile nani anatamani kurudi tena?”. “ usijali hata mimi nitarudi na k**a kuna mtu mwingine atahitaji twende nae haina shida tutaenda nae” mara GODI alilopoka tena “ mimi nitaenda tena” wote tulicheka ila nilipofikilia mara mbili mbili niligundua kwanini GODI ametaka kurudi tena, ilikua si kingine bali ni zile almasi kwenye lile pango. “ maana pale katika wale ndege tunachokihitaji sisi ni ile midomo yao na miguu yao tu ndio yenye zile sumu”.
Wote tulikubaliana na siku iliyofata ikapangwa ndio iwe siku ya kwenda kuwakusanya wale ndege na safari hii wote tulijiandaa kwenda lakini pale kambini alibaki BITE na wale wagonjwa wawili yaani DANI na Zakia ili apate kuwatibia k**a kuna tatizo lolote litajitokeza pindi sisi hatupo. Zilitolewa gari tatu ndogo na tuliwa amuru kila mmoja abebe begi lisilokua na kitu ndani na kila mmoja awe na silaha iliyoshiba risasi vilivyo, ila kwa upande wangu nilibeba mabegi mawili yaani la kwangu na la dokta BITE huku MARIAM nae akibeba mabegi mawili la kwake na la DANI kisha tukaingia ndani ya gari zetu ili safari ianze. “nyie mbona wenzetu mmebeba mabegi mawili mawili?” SALVA alituuliza mimi na MARIAM, “utajua tukishafika huko” MARIAM alimjibu kwa ufupi na kupanda ndani ya gari na kisha tukaianza safari kuelekea msituni.

ITAENDELEA.

Nicheki kwa sms au WhatsApp 0766416862 kwa mahitaji ya fulu hadithi kwa bei ya 1000/=

Address

Kigoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Abandélwa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share