19/10/2025
HADITHI : PENZI LA ABIRIA (Passenger's Love)
MTUNZI : PAUL JOHN ( PAJO )
WhatsApp Link : https://chat.whatsapp.com/B4fXcO3vppq0Uoi1TG3oB2?mode=ems_share_t
PART: 1
ILIKUWA ni asubuhi Moja tulivu siku ya Jumamosi Mbezi Stand ya Magufuli! ni kipindi cha Desemba fulani hivi Shule zikiwa zimefungwa na WAFANYAKAZI wengi wakiwa Likizo pamoja na familia zao wakitoka Mjini na kuelekea Vijijini kwa ajili ya Mapumziko pia kusherekea siku kuu za mwisho wa Mwaka.
""""""***********""""
Palitokea Jamaa mmoja hivi Mrefu kiasi kavaa Koti Jeusi na kubeba begi dogo mgongoni kwa muonekano ni mwenye umri wa kati ya 25 - 28 aliingia ndani ya Basi la PAMA TRANS linalofanya safari zake za Dar - Moro kila siku, mkononi akiwa ameshikilia tiketi yake ya safari huku akiangaza kutafuta ilipo siti yake.
Wakati akiangalia huku na kule akaiona na kuanza kuisogelea kwa ajili ya kukaa, cha kushangaza alistuka mnoo alipoifikia na kuanza kutabasamu kumbe palikuwa na Msichana mrembo kweli kweli akiwa kajifunga kilemba kichwani mwake.
Hakika alivutia na hakuweza kabisa kuboa mboni za Mzee baba kumtazama hasa kwa sura na ile rangi yake utadhani ni Malaika alietoloka Pepo na kuangukia duniani akiwa ameketi siti ya Dirishani.
Basi Mzee baba alijitaidi kulisaminisha vyema Umbo la mrembo yule hata hasiseme chochote lakini hakuweza kuling'amua vizuri kutokana alikua amevalia gauni refu la kifahari maarufu k**a Abaya.
""""""*******"""""
Jamaa alishukuru kimoyo moyo kwa kupangiwa siti pamoja na Mrembo huyo taratibu alivua begi na kukalia siti yake huku akimsalimia yule Msichana.
Hali isiyo ya kawaida yule Mrembo alimuangalia tu Mzee baba bila kumjibu chochote na akaendelea na mambo yake.
Kwa jinsi alivyomtizama jamaa alionekana kabisa ataki mazoea hivi, kisha akatoa Ear phone za rangi ya pink ktk pochi yake na kuziweka masikioni na kuanza kula burudani ya muziki kutoka kwenye simu yake. Kitendo kile kilimuumiza mnoo Mshikaji.
"""""'********"""""""
Baada ya Safari kuanza wakiwa njiani kila Mtu akiwa na hamsini zake, ghafla Simu ya Mrembo yule iliita ilikuwa namba ngeni kwake, akaipokea alisikia Sauti ya kiume bila kujua ni nani, ikimuambia kua mwisho wake umefika, anapoenda hutorudi tena na Kisha simu ikakatika.
Kiukweli yule Mrembo alishangazwa sana na Ile kauli huku mapigo ya moyo wake yakienda kasi utadhani Treni ya SGR.
Mara akazitoa zile Ear phone masikioni na kuanza kuchungulia nje ya lile BASI kwa jinsi alivyovulugwa. Pia alimkazia macho Mshikaji yule aliekuja na kukaa siti ya pembeni yake.
Kipindi icho Jamaa akili yake haikuwepo pale, ilikua mbaali sana akipanga swadi zake kichwani za kumuingia yule Mrembo.
Ikamlazimu Mrembo ainuke kuangalia ktk siti za pande zote labda angeweza kumuona aliempigia Simu k**a yupo mle au laa! lakini wala akuweza kuambulia kitu akarudi na kukalia tena siti yake.
""""*********"""""""""
Tokea pale safari ikawa ngumu na ya Uzuni kwa Mrembo yule maana ilikuwa Simu ya kutatanisha na asijue ni nani aliempigia. Alijaribu mara nyingi kuipiga Ile namba lakini waapi! maana ilikuwa haipatikani tena.
lakini kipindi anaangaika angaika, Mshikaji alistuka na kumuangalia kwa mshangao yule mrembo, huku asijue kilichomsibu.
Alipata wasiwasi alipomuona mtoto wak**e akijiongelesha mwenyewe huku sura na mboni za macho yake zikianza kuondoa nuru kwa kutandwa na machozi.
"""""*******"""""""
Mzee baba alimpiga jicho la wizi mrembo huku akijiuliza kichwani mwake ni masaibu gani tena yaliompata.
Ataanzia wapi kumuuliza kutokana alionekana ni mtu mwenye kujisikia (Slay Queen) maana hata salamu yake aliigomea kumuitikia.
Hata hivyo Mshikaji alijipa moyo kua yeye ni Mwanaume tena aliekamilika hapaswi kuogopa. Kweli alimuuliza wakati huo Mrembo alikuwa ameinamisha uso wake chini akilia.
"Samahani Mrembo kuna tatizo lolote linalokusumbua au unaumwa?" Mzee baba aliuliza huku akimshika bega
Mrembo aliinua Uso wake na kumuangalia Jamaa kwa sura iliojaa maswali mengi huku akiwa anatiliikwa na machozi ambayo yaliatibua hadi 'Make Up' yake aliokua amejipaka.
Mshikaji alipoona vile akajiandaa tayari tayari kwa shushu lolote maana alijiona k**a mtu mwenye shobo hivi kwa mrembo ambae haitaji hata ukaribu nae.
PART: 2
Kipindi Mrembo ana muangalia hajajua atapokea jibu gani Mzee baba akakumbuka ktk begi lake kuna kitambaa kipya alinunua wakati anapanda BASI pale Magufuli stand.
Hivyo akafungua Begi lake alilokua amelipakata akatoa kitambaa kile akampa yule Mrembo ili ajifute Machozi yanayomtoka.
""""""********""
Mshikaji hakuamini macho yake baada ya kuona Mrembo anakipokea kile Kitambaa na kuanza kujifuta Machozi huku bado akiendelea kulia japo sio kwa Sauti ya juu.
Basi Jamaa aliona k**a hatua Moja ya mipango yake imefanikiwa tofauti na alivyowaza. Ikabidi sasa aongeze juhudi za kumbembeleza na kumnyamazisha mrembo yule Ili amsimulie nini kimepelekea kumliza kiasi kile k**a kipo ndani ya uwezo wake aweze kumsaidia.
Kipindi mrembo akiendelea kujiifuta machozi kwa kile kitambaa, Mshikaji hakutaka kupoteza point akajiongeza fasta.
"By the way naitwa JULIUS naelekea Moro kwa ajili ya Likizo ya kikazi sijui mwenzangu unaitwa nani?" Mzee baba alijitambulisha
Yule Msichana nae alimjibu kuwa anaitwa ROSE huku Sauti yake ikitoka kwa tabu na wasiwasi mnoo kwa uoga.
"""""*******""""""""
"Kwahiyo ROSE niambie ni jambo gani linalokusumbua mama mpaka kufikia kulia?". Mshikaji ambae alijitambulisha k**a JULIUS aliuliza.
JULIUS hakuelewa na ilimshangaza zaidi kuona ROSE anatokwa zaidi na machozi baada ya kumuuliza lile swali na ingali anakumbuka tokea wanatoka pale Dar mrembo alikuwa yupo fresh tu.
Kwa Upande wa ROSE kabla hajajibu swali la JULIUS, huku machozi yakiendelea kutililika aliaangalia tena pande zote za lile BASI (PAMA TRANS) walilopanda hakuona chochote.
Kila abiria alikua bize na mambo yake hakuna alieonekana kumuhusu au kumuhisi kuhusika kwa Ile simu.
Ikambidi ROSE avute pumzi kwanza na kumuangalia JULIUS kisha akaanza kusimulia.
"Nimepokea Simu ya namba ngeni muda sio mrefu ikiniambia kuwa hii safari yangu sitaweza kurudi tena Dar na huu ndio mwisho wangu, Sasa sielewi nani alienipigia na kwanini aniambie hivi mimi?". ROSE alilalama huku akitokwa na machozi
"""""""*******""""""""
JULIUS alionekana kushangazwa na kile alichokisikia ikabidi aongeze swali lingine kwa ROSE.
" Pole sana ROSE, Lakini kwani ulipotoka huko Kuna Mtu umetofautiana nae pengine kabla hujaanza hii safari?"
ROSE alijibu "Hapana"
"Sasa k**a hapana ni nani anaweza kukupigia Simu na kukutisha ilihali hujamkosea au jaribu kumbuka vizuri uenda umesahau". JULIUS aliongeza kusema.
"Kiukweli sikumbuki kabisa uwezi amini k**a Kuna mtu nimegombana nae ama kumchukulia chochote" ROSE aljibu na kuiweka Simu yake sikioni akijaribu tena kuipiga Ile namba aone k**a atafanikiwa lakini bado haikupatikana.
Mara wazo likamjia kichwani JULIUS akamuambia ROSE wajaribu njia ya k**a kuitumia pesa hivi Ile namba watambue usajili wake Ili mrembo yule akiona Jina litakalotokea labda anaweza kukumbuka kitu.
""""""********"""""'''"
Basi wakafanya hivyo huku Safari ikiendelea wakivipita vijiji kadhaa njiani. Walifanikiwa kupata usajili wa Ile namba ROSE alipoona hakulitambua hilo jina pia akasema hajawai kulisikia kabisa ktk Masikio yake.
JULIUS akaona ajaribu kuipiga Ile namba kwa Simu yake pengine ingeita aliamini namba ya ROSE uenda aliempigia atakuwa ameiblock baada tu ya kutoa vitisho vyake.
Harakati za kujaribu kupiga Bwana JULIUS nae mambo ni yale yale tu, namba haikupatikana zaidi aliambulia kusikia tu sauti iliosetiwa na Mtandao
"Namba unayopiga kwasasa haipatikani jaribu tena baadae".
""""""******"""""
ROSE alimuuliza kwa shauku JULIUS k**a inapatikana au inaita Ile namba.
"Mambo bila bila aisee, ila tusikate tamaa tutamtafuta tena baadae, unaweza kuta Simu yake imekata chaji au network siunajuwa maeneo yenyewe tuliopo". alijibu JULIUS
ROSE alionekana mtu aliekata tamaa na kuhisi kuchanganyikiwa baada ya kusikia vile huku Joto la Uoga na Wasiwasi likizidi kupanda akihofia usalama wake.
JULIUS alijitaidi kumpa moyo na kumfanya apoteze mawazo kwa kumsimulia hadithi kadhaa zenye mfanano wa tukio lake.
Pia alimuhakikishia atamjua tu maana ana rafiki yake anafanya kazi ktk ule Mtandao wa Simu anamsaidia mambo mengi mnoo hata hilo atafanikisha mrembo asihuzunike.
"Ujue nini ROSE haya utokea sana na kwakua unasema hujamkosea mtu basi niamini, hii Simu atakua kakosea namba na k**a itakua yako basi imeisha hiyo kuna mwanangu pale town Dar anapiga kazi ktk huu Mtandao atafanikisha hutoamini". Alisema JULIUS
"Haiwezekani huyu atakua ana maanisha tu, kwanini alivyopiga nilivyopokea aongee maneno ya vitisho halafu akakata Simu na kuzima hapo hapo?!" ROSE aliongea kwa Sauti yenye gadhabu ni wazi alichukizwa mnoo na hata safari yake aliijutia sana.
PART : 3
Wakiwa ndani ya PAMA TRANS Safari ilizidi kuendelea mara ROSE alijikuta anapatwa na Usingizi. Swali. Je, ni kutokana na uchovu au Mshikaji kamfanyia umafia aweze kumfanyia kitu chochote maana hawajuani wamekutana tu safarinI.
Safari ya Dar - Moro haikuwa ya kitoto kwao hasa mtu ukisafiri kwa BASI. Wakiwa wanavipa Mgongo vijiji kadha wa kadha Mvua nayo ilianza kunyesha na kudumu nayo kwa muda kidogo wakiwa njiani na hali ya hewa kubadilika pakawa na kaubaridi hivi.
JULIUS alipoona kwa vile alikuwa amevaa Koti ndani tisheti basi alilivua lile Koti na kumfunika ROSE ambae alikuwa bado amesinzia.
Uwezi amini kwa jinsi ROSE alivyolegea na kumuegemea JULIUS udhanii kabisa k**a ni yule aliigomea hata Salamu yake.
""""""*********""""
Ghafla ROSE aliamka baada ya kustushwa na makelele ya honi za Magari, alifumbua macho yake malegevu taratibu k**a mtu aliekula kungu manga alijikuta kumbe muda wote ule aliolala alikuwa ameegemea bega la JULIUS.
Akainua kichwa fasta huku akijiweka vizuri kilemba chake alichokuwa amejitanda kichwani na alionekana mtu mwenye kujistukia kwa kitendo kile cha kulala begani kwa Mzee baba.
Maana akutegemea na akaanza kuzuga akiangalia angalia dirishani na kujiongelesha.
" Kumbe tumeshafika Moro, nilikuwa nimepitiwa na Usingizi aisee?" daa! uchovu huu!!".
JULIUS alibakia akitabasamu tu huku akimuangalia ROSE anavyojimaliza mwenyewe, alitamani safari ingekuwa bado inaendelea ili Mrembo aendelee kuegemea bega lake, maana alijihisi k**a muvi hapo staring ameshinda vita anarudi kambini na mateka wa k**e aliemuokoa na kifo.
"""""******"""""
Mara PAMA TRANS likasimama pale ndani Msamvu Stand. ROSE, JULIUS na abiria wengine walianza kushuka.
Cha ajabu ROSE alionekana mwenye furaha sana sijui kutokana na stori za Mshikaji zilimsaidia kumsahaulisha matatizo yake au alifanikiwa kupata msaada wa huyo Jamaa wa town alieambiwa na JULIUS.
Maana k**a mtu anaefanikiwa kuwaona kwa mara ya kwanza hapo angejua walikuwa wanaenda sehemu moja au watu wanaofahamiana kwa muda mrefu kwa jinsi walivyokuwa wakionekana.
JULIUS alimwambia ROSE kwakua wamefika salama inabidi huko anapoenda apitie kituo cha Polisi aweze kuwaelezea kilichotokea, kwakua Polisi wana mafunzo na mbinu za kutambua Wahalifu itakuwa rahisi kumsaidia na salama kwake ama kulikalia kimya.
""""""******""""""''
ROSE alikubaliana na lile wazo maana awezi juwa kua aliempigia simu alimuacha Dar au atakutana nae hapo Morogoro. Kabla ya kuagana na kila Mtu aelekee safari yake walipeana namba za Simu.
JULIUS alimwambia ROSE kuwa yeye anaelekea BiGWA ndipo asili yake ilipo yaan Wazazi wake wanaishi huko.
"Mimi naelekea zangu KIHONDA ndipo Baba yangu anapoishi ila mama yangu ni Mzigua wa Handeni Tanga. Halafu kabla sijasahau uliniambia una rafiki yako anafanya kazi ktk hiyo kampuni ya mawasiliano anaweza kusaidia, utongea nae basi anisaidie hata pesa nitampa" Alisema ROSE
"Ondoashaka mrembo, huyo ashindwi na kitu tena jambo k**a ilo mbona dogo kwake utafurahi mwenyewe niamini" JULIUS alisema
Basi wakakumbatiana na kila mtu alielekea njia yake na waliahidiana kutafutana tena kujua majibu ya huyo rafiki yake JULIUS wa kampuni ya mawasiliano huko Dar.
Juma pili ijayo itaendelea.....